IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya wanajeshi wa Iran

15:31 - December 11, 2011
Habari ID: 2236538
Naibu Mkuu wa Kituo cha Darul Qur'ani katika Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema wanajeshi 600 watashiriki katika Mashindano ya 31 ya Kitaifa ya Qur'ani ya Wanajeshi nchini baadaye mwezi huu.
Kapteni Mehdi Meydani amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa mashindano hayo yataanza Jumatatu 19 Disemba katika makao makuu ya jeshi mjini Tehran.
Amesema washiriki ni kati ya walioshinda katika mashindano ya mchujo ya Qur'ani ya vikosi vya nchi kavu, anga, na wanamaji.
Kapteni Meydani ameongeza kuwa washiriki watashindana katika vitengo vya tarteel, hifdhi ya juzuu 3, 4, 5, 10, 20 na 25 pamoja na kuhifadhi Qur'ani kamili. Aidha kutakuwa na mashindano ya adhana.
Ameongeza kuwa washindi wa vitengo mbalimbali watatangazwa na kutunukiwa zawadi Jumatano Disemba 21.
912515
captcha