Mkutano huo unafanyika kwa ushirikiano wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Malaysia na Shirika la Sayansi, Elimu na Utamaduni la Kiislamu (ISESCO) na utaendelea na kazi zake hadi tarehe 15 Disemba.
Wawakilishi wa nchi za Indonesia, Singapore, Brunei Ufilipino, Jamhuri ya Maldives, India, Pakistan na Bangladesh, viongozi wa vyuo vikuu vya Qur'ani kutoka nchi za Saudi Arabia, Ghana, Misri, Tajikistan na Yemen na vilevile wawakilishi 15 wa vyuo na taasisi za utafiti wa Kiislamu na Qur'ani wa Malaysia wanashiriki katika mkutano huo.
Miongoni mwa malengo ya mkutano huo ni kukuza kiwango cha utafiti wa masuala ya Qur'ani na kupanga ratiba ya shughuli kama hizo, kutathmini shughuli za taasisi za Qur'ani katika nchi zinazoshiriki katika mkutano huo na kubadilishana uzoefu katika kutoa mafunzo ya Qur'ani. 914038