IQNA

Mashindano ya kuhifadhi Qur'ani kufanyika Riyadh

23:45 - December 12, 2011
Habari ID: 2237418
Awamu ya 14 ya Mashindano ya Qur'ani ya Salman bin Abdulaziz ya wavulana na wasichana yatafanyika 27 Februari na 4 Machi mwakani kwa taratibu.
Waziri wa Masuala ya Kiislamu na Waqfu nchini Saudia Sheikh Saleh bin Abdulaziz Al Al-Sheikh ameidhinisha mpango huo wa awamu ya 14 ya Mashindano ya Qur'ani ya Salman bin Abdulaziz ya wavulana na washichana.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Saudia SPA, lengo la mashindano hayo ni kuakisi na kuonyesha azma ya Saudi Arabia katika masuala ya Qur'ani Tukufu.
Aidha mashindano hayo yanakusudia kuonesha namna Saudi Arabia inavyojali masuala ya hifdhi na qiraa sahihi ya Qur'ani tukufu. Mashindano hayo pia yanalenga kuwapa motisha na kuwahimiza wavulana na wasichana wadogo kuhifadhi Qur'ani.
914030
captcha