Lengo la wiki hiyo ni kuarifisha mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu na mchango wa Iran katika upeo wa kimataifa. Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, hafla hiyo itafanyika Februari 1-12 mwakani katika Kituo cha Utamaduni cha Iran mjini Khartoum.
Katika kipindi hicho, washiriki wataweza kujifunza kuhusu Mapinduzi ya Kiislamu, sala, Qur'ani, fasihi ya Kifarsi na huduma zake kwa Uislamu, muqawama, mwamko wa mataifa na ukuruba baina ya madhehebu ya Kiislamu.
Aidha kutakuwa na maonyesho ya kisayansi, kisiasa, kijami, wanawake na watoto nchini Iran. Vilevile makundi ya muziki wa kiutamaduni na wanakaligrafia kutoka Iran watawasilisha sanaa zao katika maonyesho hayo.
913507