IQNA

Sayyid Nasrullah, Tumaini la Wapalestina

23:32 - December 12, 2011
Habari ID: 2237421
Sayyid Hassan Nasrullah, Kiongozi wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon ndie tumaini la Wapalestina katika kuikomboa Quds Tukufu kutoka kwenye makucha ya Wazayuni maghasibu.
Hayo yamesemwa na Ali Suweydan mwanachama wa zamani wa Harakati ya Fat'h ya Palestina. Katika mahojiano na IQNA, Suweydan amesema Nasrullah daima amekuwa akisimama bega kwa bega na taifa la Palestina na amechukua misimamo imara kabisa katika kuunga mkono harakati za ukombozi za Wapalestina.
Ameashiria nafasi ya harakati ya mapambano ya Hizbullah inayoongozwa na Sayyid Nasrullah kwa kusema: "Tokea ianzishwe, Hizbullah imeliletea taifa la Lebanon ushindi mara kadhaa. Hizbullah ina nafasi kubwa katika ulimwengu wa Kiislamu kutokana na mapambano yake yenye thamani. Hizbullah imeleta mafanikio katika mataifa ya Kiarabu na Kiislamu na sasa ni harakati mashuhuri miongoni mwa Waislamu".
Suweydan amesema kuwa Hizbullah imekuwa na nafasi muhimu katika kuimarisha umoja nchini Lebanon. Ameongeza kuwa Hizbullah imeweza kuwalunganisha Waislamu katika mapambano yao dhidi ya utawala wa Kizayuni ambao ndio adui mkubwa zaidi wa umma wa Kiislamu.
913214
captcha