IQNA

Maonyesho ya athari na picha za Waislamu wa kwanza nchini Australia yafanyika Malaysia

14:40 - December 13, 2011
Habari ID: 2237820
Maonyesho ya athari na picha za Waislamu wa mwanzoni nchini Australia yanaendelea katika jumba la maonyesho la Sanaa ya Kiislamu IAMM mjini Kuala Lumpur, Malaysia.
Kwa mujibu wa tovuti ya Islam Today, maonyesho hayo yataendelea hadi tarehe 21 Januari. Maonyesho hayo yanazungumzia Waislamu walioacha nchi zao kwa madhumuni ya kutafuta na kugundua ardhi mpya huko Austarlia. Kwa ibara nyingine, Waislamu hao walikuwa miongoni mwa watalii wa kwanza kabisa kufika Australia.
Maonyesho hayo yanajumuisha kazi za mikono, picha, michoro na nyaraka mbalimbali zinazothibitisha safari na maisha ya Waislamu huko Australia tangu zama za kale. Nguo, miswala, tasbihi, silaha na vitabu vya kale vya Kiislamu ni miongoni mwa athari hizo.
Vilevile kwenye maonyesho hayo kuna picha za kuvutia za kale zilizo na umri wa zaidi ya karne moja, zikiwemo zile zinazoonyesha wachungaji wa ngamia wakiwa wamesimama pembeni ya ngamia hizo.
Inasemekana kuwa zaidi ya miaka 150 iliyopita misafara mikubwa ya Waislamu walioandamana na ngamia zao, kutoka nchi za Afghanistan na India ilihamia Australia kwa sababu tofauti na kuanzisha huko kizazi kipya cha Waislamu. 914309
captcha