Kwa mujibu wa Ali Ezzati Mkurugenzi wa Elimu wa jiji la Tehran, madrasa hiyo itajengwa eneo la kusini magharibi mwa Tehran. Akizungumza na IQNA, amesema ujenzi wa madrasa hiyo utaanza mwezi Februari mwakani kwa mnasaba wa maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Amesema kiwanja chenye ukubwa wa 22,000 mita mraba kimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa madrasa hiyo. Ameongeza kuwa usanifu majengo wa Kiislamu-Kiirani utatumika kujenga madrasa hiyo.
Wakaazi wa Tehran na maeneo mengine ya Iran watapata fursa ya kunufuka na mipango ya masomo ya Qur’ani katika chuo hicho, amesema. Bw. Ezzati amedokeza kuwa madrasa hiyo itatoa mafunzo katika viwango tafauti na kwamba wanafunzi watapata mafunzo ya Qur’ani Tukufu kuhusu kuhifadhi, kusoma, tafsiri, tarjuma n.k.
Ali Ezzati amearifu kuwa chuo hicho kitakuwa na ukumbi wa filamu aina ya 5D kwa lengo la kuonyesha filamu zinazohusu Qur’ani Tukufu.
914397