IQNA

Iran ilikuwa ya kwanza kuanzisha sukuk

22:29 - December 13, 2011
Habari ID: 2238290
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilikuwa nchi ya kwanza duniani kuanzisha hati za dhamana za Kiislamu yaani sukuk katika soko la kifedha, amesema mtaalamu wa uchumi mjini Tehran.
Akizungumza na Radio Iqtisad (uchumi), Mohammad Sajjad amesema kwa mwaka 1997 Iran ilifanikisha ujenzi wa Barabara Kuu ya Navab mjini Tehran kwa kutumia sukuk.
Amesema Iran ilianzisha mfumo maalumu wa kusambaza sukuk mwaka 1994 na kuwasilisha mfumo huo katika Kongamano la Pili la Banki za Kiislamu mwaka huo.
Mohammad sajjad ameongeza kuwa baadhi ya mashirika hufadhili miradi yao kwa kupitia kuuza hisa n.k na kuongeza kuwa hati za dhamana za Kiislamu au sukuk, pia zinaweza kutumika kufadhili miradi.
Sukuk ni neno la Kiarabu la vyeti vya kifedha na huashiria hati za dhamana za Kiislamu. Kutokana na kuwa hati za dhamana ambazo hutozwa riba haziruhusiwi katika Uislamu, sukuk huzingatia sheria za Kiislamu.
Kwa mujibu wa wataalamu wa kifedha, soko la sukuk situ kuwa ni sekta inayokuwa zaidi katika mfumo wa kifedha wa kiislamu bali pia ni kitengo kinachostawi kwa kasi zaidi katika masoko ya kifedha duniani.
914561
captcha