Kwa mujibu wa gazeti la as-Sharqul Ausat, viongozi wa Morocco wamesema kuwa mpango huo utahusu ujenzi wa shule zinazofanana na za mafunzo ya fiqhi na misingi ya dini katika miji tofauti ya nchi hiyo. Kimsingi shule hizo zilikuwa zikitumika zamani katika maeneo ya vijijini na yaliyo mbali na miji.
Watekelezaji wa mpango huo wanatumai kwamba shule hizo hazitakuwa zikitoa mafunzo ya kidini tu bali zitabadilika na kuwa vituo muhimu vya elimu nyinginezo za kisasa, ambazo zitasimama kwenye msingi wa mafunzo ya Kiislamu.
Shughuli za shule za Kiislamu nchini Morocco hutofautiana kutoka eneo hadi jingine, kwa maana kwamba, baadhi ya shule hizo hujishughulisha na mafunzo ya Qur'ani na Hadithi tu ilhali nyingine huongeza kwenye masomo hayo masomo mengine ya kiakademia yakiwemo ya hesabati, lugha ya Kiarabu, historia na jiografia.
Vilevile katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo shule hizo mbali na kusimamisha swala na ibada za kidini hujishughulisha na mambo mengine ya kijamii, michezo na mazoezi ya mwili. 915155