Amesema kuwa katika Hija ya mwakani, inshaAllah, huduma bora zaidi zitatolewa kwa mahujaji baada ya kuchunguza udhaifu uliokuwepo katika Hija iliyopita.
Amesema kuwa Wairani 97,000 walishiriki katika ibada ya Hija wakiwa katika makundi 596. Ameongeza kuwa oparesheni ya kuwasafirisha mahujaji ilitekelezwa na mashirika mawili ya ndege ya Homa na Mahan. Ameongeza kuwa Ofisi ya Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ilionyesha ushirikiano bora katika kuhakikisha Wairani wanafanikiwa katika ibada ya Hija.
'Katika mkutano na Waziri wa Hija wa Saudi Arabia, waziri alipongeza nidhamu ya mahujaji Wairani', amesema Layali.
Aidha afisa huyo mwandamizi wa Hija ameshukuru mashirika ya ndege ya Iran, Idara ya Polisi, Wizara ya Mambo ya Nje, timu za madaktari na mashirika mengine yaliyofanyikisha ibada ya Hija. 915392