IQNA

Mfumo wa fedha wa Kiislamu wastawi Afrika Mashariki

9:58 - December 18, 2011
Habari ID: 2240336
Baada ya kufunguliwa Benki ya Kiislamu ya Amana nchini Tanzania, mfumo wa kifedha wa Kiislamu Afrika Mashariki unazidi kuimarika.
Kwa mujibu wa tovuti ya intaneti ya CPI Financial, Asad Ahmad Mkurugenzi wa Gulf African Bank, Benki ya kwanza ya Kiislamu nchini Kenya amesema mfumo wa Kifedha wa Kiislamu unazidi kupanuka Afrika Mashariki.
‘Katiba mpya imepitishwa Kenya, Tanzania imefungua benki yake ya kwanza ya Kiislamu na Uganda imepitisha sheria ya kuruhusu benki za Kiislamu na tayari taasisi tatu nchini humo zimeomba idhini ya kuanzisha huduma za kifedha za Kiislamu’, amesema Ahmad.
Ameongeza kuwa Gulf African Bank inalenga kupanua shughuli zake hadi Tanzania na Uganda baada ya kuimarika nchini Kenya. ‘Mfumo wa kifedha wa Kiislamu Afrika Mashariki ni fursa ya kuonyesha kuwa mfumo wa benki wenye maadili unaweza kufanya kazi katika eneo hili’. Mkuu huyo wa Gulf African Bank nchini Kenya amesisitiza kuwa huduma za benki za Kiislamu si kwa ajili ya Waislamu pekee bali kwa watu wote wanaovutiwa na utendaji kazi bora wa benki za Kiislamu.
Naye Rais wa Zanzibar Ali Mohammad Shein hivi karibuni alitoa wito kwa Benki ya Tanzania kuanzisha huduma za Kiislamu.
917151
captcha