IQNA

Awamu ya pili ya wafungwa wa kipalestina yaachiwa huru

8:26 - December 19, 2011
Habari ID: 2241069
Wafungwa na mateka 550 wa Kipalestina walioachiliwa huru na utawala wa Kizayuni wa Israel wamewasili katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Gaza.
Kuachiliwa huru Wapalestina hao kumefanyika katika fremu ya awamu ya mwisho ya makubaliano ya kubadilishana mateka yaliyofikiwa kati ya mamlaka ya ndani ya Palestina, Harakati ya Hamas na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Itakumbukwa kuwa zaidi ya Wapalestina 470 waliokuwa wakishikiliwa kwenye magereza ya kuogofya ya utawala wa Kizayuni waliachiwa huru sambamba na kukabidhiwa utawala haramu wa Israel askari wake mmoja Gilad Shalit aliyekuwa akishikiliwa mateka na wanamapambano wa Hamas katika awamu ya kwanza ya zoezi hilo.
Kuachiliwa huru kwa wafungwa wengine 550 wa Kipalestina kunaifanya idadi ya Wapalestina walioachiliwa huru kutoka katika magereza ya kuogofya ya Wazayuni kufikia 1,027 na huo ni ushindi mwingine wa kusimama kidete wanamapambano wa Palestina. 917346
captcha