Kwa mujibu wa tovuti ya espacemanager, Rais Marzouqi alizungumza na kujadiliana na viongozi hao kuhusu mambo na matatizo yanayowatatiza wafauasi wa dini tofauti nchini.
Akizungumza na waandishi habari mara tu baada ya kumalizika mazungumza hayo, Sheikh Othman Battwikh, Mufti Mkuu wa Tunisia amesema kuwa moja ya mambo yaliyojadiliwa katika kikao hicho na Rais Marzouqi ni pamoja na kutafutwa njia za kuelekeza, kuongoza na kuwavutia wananchi zaidi kwenye dini na kuarifishwa sura halisi ya Uislamu pamoja na kuimarishwa amani na uadilifu katika jamii.
Kwa upande wao viongozi wa Kiyahudi na Kikristo wamesema kuwa mazungumzo hayo yalikuwa ya kihistoria na kwamba Rais Marzouqi aliwataka wafuasi wa dini hizo ambao huenda walikimbia nchi hiyo kutokana na sababu za kisiasa warejee nchini na kuishi pamoja kwa amani na wenzao ili kustawisha nchi hiyo kimaendeleo.
Wamesema Rais Marzouqi amewataka wafuasi wa dini hizo kuishi pamoja kwa amani na wenzao wa Kisilamu bila kuwepo aina yoyote ya chuki na uadui. 919118