Insaiklopidia hiyo imetayarishwa na Gholam Reza Heydari Abhari na Roya Khoi. Ni mjumuiko wa makala kutoka vyanzo vya Kiarabu na Kiingereza.
Makala hizo zinafafanua istilahi za Kiislamu na kuarifisha shakhsia wa kidini. Aidha insaiklopidia hiyo inawaarifu wasomaji kuhusu matukio muhimu katika historia ya Iran.
Insaiklopidia ya Kiislamu ya Watoto itachapishwa kwanza katika juzuu moja.
Insaiklopidia hiyo itazinduliwa katika Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu Tehran yanayotazamiwa kufanyika Mei 2012.
919206