Mada kuu katika kongamano hilo ni ‘Ustawi Endelevu na Maendeleo ya Kiuchumi yanayowahusisha watu wote kwa mtazamo wa Kiislamu’.
Kongamano hilo linawakutanisha pamoja wataalamu wa uchumu, wakuu wa benki kuu, wahadhiri waandamani na watafiti kutoka nchi 35 ambao wamewasilisha makala 130 za utafiti katika nyuga mbalimbali kuhusu benki za Kiislamu,masoko na upeo wa uchumi wa Kiislamu. Aidha suala la huduma za kifedha katika nchi za Kiislamu na hatua za nchi hizo katika Malengo ya Milenia ya Umoja wa Mataifa ni katika ya mada zilizojadiliwa.
Kongamano hilo limeandaliwa na Kituo cha Masomo ya Kiislamu cha Qatar, Taasisi ya Utatifi na Mafunzo ya Kiislamu, Benki ya Maendeleo ya Kiislamu, Benki Kuu ya Qatar na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu.
919446