IQNA

Njia za kuboresha shule za Kiislamu kujadiliwa Mali

18:57 - December 21, 2011
Habari ID: 2243055
Kikao cha mafunzo ya kuboresha shule za Kiislamu na Kiarabu kimepangwa kufanyika tarehe 26 hadi 29 Disemba katika mji mkuu wa Mali, Bamako.
Kikao hicho kitasimamiwa na shirika la Kiislamu la Elimu, Sayansi na Utamaduni ISESCO na taasisi ya al Muntada al Islami ya London.
Maafisa 20 wa shule za Kiislamu kutoka nchi za Algeria, Senegal, Guinea Bissau, Guinea Conakry, Burkina Faso, Morocco, Mauritania na Mali watashiriki katika kikao hicho.
Lengo la kikao hicho cha kieneo ni kuarifisha historia ya kuanzishwa shule za Kiislamu, mchango wake katika kueneza elimu mbalimbali katika karne zilizopita, uchunguzi wa matatizo ya elimu, sayansi, uchumi na uongozi wa shule za Kiislamu na njia za kuboresha kiwango cha shule hizo. 919991
captcha