Hizbullah imesema kuwa hujuma hizi za kigaidi zimetekelezwa kwa uungaji mkono wa Marekani nyuma ya pazia.
Hizbullah imesema hujuma hizo za mabomu zilikuwa za makusudi kwa lengo la kudidimisha sherehe za Wairaqi katika siku za awali za kuondoka vikosi vamizi vya Marekani nchini humo.
Siku ya Alkhamisi kwa akali watu 63 waliuawa na zaidi ya 170 kujeruhiwa baada ya kutokea miripuko kadhaa ya mabomu katika maeneo mbalimbali ya mji huo.
Maafisa wa usalama wamesema kuwa mashambulizi hayo yalikuwa yamepangwa kwani yalitokea kwa wakati mmoja. Mashambulizi hayo yametokea siku chache baada ya kundi la mwisho la wanajeshi wa Marekani kuondoka nchini humo.
Weledi wa siasa za Iraq wanaitakidi kuwa fujo zinazoshuhudiwa kwa sasa nchini humo zimeratibiwa na Marekani ili kuuhadaa ulimwengu kwamba Iraq haina uwezo wa kudhamini usalama wake.
Huku hayo yakijiri, Waziri Mkuu wa Iraq Nouri Al-Maliki ameitaka mamlaka ya ndani ya Kikurdi imkabidhi kwa vyombo vya sheria Makamu wa Rais wa nchi hiyo Tariq al-Hashimi anayekabiliwa na tuhuma za ugaidi. Al-Hashimi anadaiwa kutoa amri ya kuuawa wapinzani wake lakini amekanusha madai hayo na kusisitiza kuwa yamechochewa kisiasa.
920781