Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP askari hao walichukua hatua hiyo ya kiukandamizaji baada ya kuvunja maandamano ya Wabahraini waliokuwa wakiandamana kwa amani kupigania haki zao katika mji huo. Askari hao walishambulia raia kwa kutumia risasi za plastiki na gesi za kutoa machozi.
Chama cha al-Wifaq kimetoa taarifa kikisema kuwa shambulio la askari hao katika makao makuu ya chama hicho lilifanyika wakati wanachama wa chama hicho walipokuwa wakifanya kikao cha kila wiki. Wanachama na raia kadhaa akiwemo mwandishi habari wa Marekani walijeruhiwa katika shambulio hilo la kichokozi.
Awali Wizara ya Mambo ya Ndani ya Bahrain ilipiga marufuku vikao vya chama cha al-Wifaq katika makao makuu hayo kwa hoja kuwa kinapinga utawala wa Aal Khalifa. 921111