IQNA

Hizbullah yaituhumu Marekani kuhusika na mashambulizi ya kigaidi Syria

13:07 - December 25, 2011
Habari ID: 2244397
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon, Hizbullah imeituhumu Marekani kwamba ilihusika na mashambulizi ya kigaidi yaliyotukia juzi katika mji mkuu wa Syria, Damascus.
Taarifa ya Hizbullah imesema kuwa, Washington, ambaye ni mama wa ugaidi imehusika katika mashambulizi hayo yaliyosababisha vifo vya makumi ya watu na wengine wengi kujeruhiwa.
Taarifa ya Harakati ya Mapamabano ya Kiislamu ya Lebanon imeongeza kuwa, Marekani imechangia kufanyika mashambulizi hayo ya kigaidi kama njia mojawapo ya kulipiza kisasa, kutokana na kufeli kwa sera na siasa zake katika eneo la Mashariki ya Kati.
Kwa akali, watu 55 walipoteza maisha yao na wengine wengi kujeruhiwa kwenye miripuko miwili ya mabomu karibu na jumba moja la vikosi vya usalama katika eneo la Kafr Sousa mjini Damascus.

921078
captcha