IQNA

Iran yasema madai ya Marekani hayana msingi

12:00 - December 25, 2011
Habari ID: 2244593
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameyataja kuwa yasiyo na msingi madai yaliyotolewa hivi karibuni ya Marekani kuwa eti Iran ilihusika na hujuma za Septemba 11.
Alkhamisi iliyopita jaji mmoja wa Marekani huko Manhattan alidai kuwa Iran ilihusika na hujuma za Septemba 11 mwaka 2001 kwa kushirikiana na Taliban na al-Qaeda.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Ramin Mehmanparast amesema Marekani inahatarisha amani na usalama wa kimataifa kwa kutoa madai kama hayo yasiyo na msingi. Amesema nafasi ya Marekani katika kuanzisha na kuunga mkono mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda ni jambo linalofahamika na wote.
Mehmanparast amesema Iran inaamini kuwa dunia inapaswa kuzingatia natija ya tabia ya kutowajibika watawala wa Marekani. Ameitaka jamii ya kimatiafa iwasilishe wasi wasi wake kwa utawala wa Marekani.
921981
captcha