IQNA

Ikwanul Muslimin yashinda awamu ya pili ya uchaguzi Misri

13:11 - December 25, 2011
Habari ID: 2244598
Kamati ya uchaguzi Misri imesema vyama vya Kiislamu vimeshinda asilimia 65 ya kura katika awamu ya pili ya uchaguzi wa bunge nchini humo.
Harakati ya Ikwanul Muslimin kupitia Chama cha Uhuru na Uadilifu kimepata asilia 36.5 ya kura zilizopigwa huku chama cha An-Nuur kikipata asilimia 28.78. Awamu ya tatu ya uchaguzi wa Bunge itafanyika Januari tatu na baada ya hapo kutafanyika uchaguzi wa Baraza la Seneti ambao nao pia ulikuwa na awamu tatu.
Wananchi wa Misri wamepiga kupiga kura huku machafuko yakiendelea kushuhudiwa kati ya waandamanji na wanajeshi wanaotawala Misri hivi sasa. Wamisri wanataka baraza la kijeshi likabidhi madaraka ya nchi kwa serikali ya kiraia.
Nukta muhimu kuhusiana na uchaguzi wa sasa wa Bunge la Misri ni kwamba, wananchi wa nchi hiyo wameuchagua Uislamu kuongoza nchi yao kati ya makumi ya vyama vyenye mielekeo ya kitaifa, kisalafi na ile ya mrengo wa kushoto. Matokeo ya awamu ya kwanza na ya pili ya uchaguzi wa bunge la nchi hiyo yanaonesha kwamba Wamisri wamerejea katika utambulisho wao wa Kiislamu. Hakuna shaka kuwa matokeo hayo yatajikariri tena katika awamu ya tatu ya uchaguzi huo mwakani.
Aidha ushindi mtawalia waliopata wanaharakati wa Kiislamu katika chaguzi za miezi ya hivi karibuni huko kaskazini mwa Afrika unaonesha ni kiasi gani wananchi Waislamu wa nchi hizo walivyoamka na jinsi siasa za kupinga dini za maadui wa Uislamu zilivyoshindwa licha ya kuendesha kampeni za karne nyingi za kupinga Uislamu. Chama cha an Nahdha nchini Tunisia kimeanza kuweka historia ya kuwa chama cha kwanza cha Kiislamu kupata ushindi mkubwa katika nchi za kaskazini mwa Afrika. Wanaharakati wa Kiislamu wameonyesha pia kuwa wana nafasi muhimu huko nchini Morocco. Chama cha Kiislamu cha Uadilifu na Ustawi kimefanikiwa kupata kura nyingi katika uchaguzi wa Bunge uliofanyika hivi karibuni nchini humo.
921969
captcha