Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, maonyesho hayo yataandaliwa na Jumuiya ya Wachapishaji Qum kwa ushirikiano na Wizara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu. Maonyesho hayo ya siku sita yatahudhuriwa na wachapishaji kutoka Lebanon, Misri, Iraq na nchi zingine za Kiislamu kuanzia Januari 12-17.
Aidha maonyesho ya kimkoa ya vitabu huko Qum yatafanyika Februari 11-19 ambapo wachapishaji 150 watashiriki.
Vile vile Jumuiya ya Wachapishaji Qum imesema itaandaa maonyesho ya vitabu maalumu kwa watoto na mabarobaro mkoani humo.
Jumuiya hiyo ilianza shughuli zake miaka 31 iliyopita na sasa ina wanachama karibu elfu moja.
922089