Mkuu wa Taasisi ya Allamah Fadhlullah amesema mashambuzi hayo yaliyofanywa na kundi lenye misimamo mikali yanakwenda kinyume na mafundisho ya Kiislamu na kwamba harakati za makundi kama hayo ya kigaidi hazipaswi kuhusishwa na Uislamu.
Ameongeza kuwa mashambulizi yaliyofanywa na kundi hilo lenye misimamo mikali hayana uhusiano wa aina yoyote na Uislamu na Waislamu na watekelezaji wake hawaheshimu mafundisho ya dini hiyo tukufu.
Sayyid Ali Fadhlullah amesisitiza juu ya udharura wa kuitishwa mkutano wa kimataifa wa Waislamu na Wakristo kwa ajili ya kulaani harakati kama hizo za kigaidi.
Makumi ya watu waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika mashambulizi ya mabomu yaliyofanywa na kundi la Boko Haram katika mji mkuu wa Nigeria katika siku ya Krismasi. 923818