IQNA

Maimamu wa Misikiti ya Russia wapata mafunzo zaidi

14:49 - December 31, 2011
Habari ID: 2248104
Maimamu wa misikiti ya eneo la Penza nchini Russia wanapata mafunzo maalumu kuhusu sayansi za kidini katika Msikitu Mkuu wa Mji wa Kuznetsk.
Kozi hiyo ya masaa 98 imepangwa na kuratibiwa na Idara ya Masuala ya Waislamu ya Russia.
Kozi kama hizo za kielimu nchini Russia hufanyika kwa ushirikiano na Waqfu wa Kuunga Mkono Utamaduni wa Kiislamu, Sayansi na Elimu.
Idara ya Masuala ya Waislamu Russia imetangaza kuwa lengo la kozi hiyo ni kuinua kiwango cha elimu na ujuzi cha Maimamu kuhusu masuala ya kidini, kiutamaduni, na kimaanawi. Kozi hiyo ilianza Disemba 19 na kumalizika Disemba 31. Imekuwa ikifanyika kila mwaka tokea mwaka 2008.
924434
captcha