Kwa mujibu wa Taasisi ya Kukusanya na Kuchapisha Athari za Imam Khomeini, takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya watu waliotembelea nyumba hiyo kuanzia Machi mwaka 2011 imefika laki tatu.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo watalii hao ni wa hapa nchini na kimataifa.
Ripoti hiyo imesema kuwa kuna programu kadhaa kwa ajili ya wageni wanaotembelea nyumba hiyo zikiwemo za kiutamaduni, maonyesho ya vitabu, kaligrafia, maonyesho ya nakshi n.k.
Mji wa Khomein ndiko alikozaliwa mwanzilishi wa Jmahuri ya Kiislamu ya Iran, Imam Ruhullah al Mousavi al Khomeini. Mji huo uko kati mwa Iran umbali wa kilomita 325 kutoka Tehran.
924636