Kwa mujibu wa tovuti ya Tembo Interactive, mamia ya watu kutoka katika vijiji vya karibu na shule hiyo walishambulia na kisha kuteketeza kwa moto jengo la shule hiyo.
Mara tu baada ya kushambuliwa shule hiyo, Taasisi ya Ahlul Beit (as) ambayo ndiyo inayoisimamia ilikosoa vikali hatua ya polisi ya kukaa kimya na kutochukua hatua yoyote ya kukabiliana na kitendo cha wahujumu.
Kuhusu jambo hilo, Abdallah Jafarino, afisa anayesimamia masuala ya kisheria katika taasisi hiyo amehoji ni kwa nini polisi haikuchukua hatua yoyote ya kukabiliana na hujuma hiyo licha ya kuwa ilikuwa na habari za kutosha kabla ya kutokea kwake? Amesema mashinikizo ya watu wenye misimamo ya kupindukia mipaka dhidi ya Waislamu wqa madhehebu ya Shia wa eneo hilo yamekuwepo kwa muda mrefu.
Idadi ya Mashia nchini Indonesia inakisiwa kuwa watu milioni mbili kati ya jamii ya nchi hiyo iliyo na idadi kubwa zaidi ya Waislamu duniani. 925761