IQNA

Kikao cha Uislamu, Ueneaji na Chuki dhidi yake kufanyika Ufaransa

11:31 - January 01, 2012
Habari ID: 2248906
Kikao cha Uislamu na jinsi unavyoenea pamoja na chuki zinazoenezwa dhidi yake na maadui kimepagwa kufanyika hivi karibuni Paris mji mkuu wa Ufaransa.
Abdul Latif Idrissi, mhadhiri wa vyuo vikuu vya Ufaransa, Francois Abrougeh, Mkuu wa Taasisi ya Mashariki ya Karibu ya Ufaransa na Nilufer Gole, Mkuu wa Utafiti katika Kituo Kikuu cha Utafaiti wa Kijamii ni miongoni mwa watu walioalikwa kuzungumza katika kikao hicho.
Maana inayokusudiwa na Wamagharibi kuhusu mielekeo ya Kiislamu, sababu za kuenea chuki dhidi ya Uislamu na chanzo cha kuenea kwake nchini Ufaransa na nchi nyingine za Ulaya, kubadilishana mawazo kuhusiana na msimamo wa wananchi wa Ufaransa kuhusu Uislamu na Waislamu na uchambuzi wa msimamo huo ni baadhi ya mambo yatakayojadiliwa katika kikao hicho. 926476
captcha