IQNA

Wabunge Waislamu Uingereza wanyimwa chakula halali

15:59 - January 02, 2012
Habari ID: 2249694
Bunge la Uingereza limewakera wabunge Waislamu baada ya migahawa katika bunge hilo kukataa kuandaa vyakula halali.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mjumbe Nazir Ahmad wa Rotherham amekerwa na uamuzi huo na kusema, 'chaguo la chakula halali linapaswa kuwepo'.
Suala hilo limegongwa vyombo vya habari baada ya idara ya Bunge la Uingereza kukataa ombi la wabunge Waislamu la kuwepo vyakula halali katika migahawa yote 23 ya bunge.
Wabunge Waislamu Uingereza wamefahamishwa kuwa hawawezi kupata nyama halali iliyochinjwa kwa misingi ya Kiislamu kwa vile eti suala hilo litawaudhi wabunge wasio kuwa Waislamu.
Sasa inasubiriwa kuona wabunge hao Waislamu nchini Uingereza watachukua hatua gani kutetea haki zao katika nchi ambayo inadai kuwa kitovu cha demokrasia na uhuru. Kuna karibu Waislamu milioni mbili nchini Uingereza.
927413
captcha