Kwa mujibu wa tovuti ya rtl, Kituo cha Kiislamu cha Ayatullahil Udhma Khui, duka la Waislamu, kituo cha ibada cha Wahindu na Kanisa la Wakristo ni miongoni mwa sehemu zilizoshambuliwa na watu hao.
Kituo cha Ayatullah Khui kimetoa taarifa kupitia mtandao wake kikisema kwamba watu hao walirusha mada za moto kwenye mlango mkuu wa kituo hicho wakiwa na lengo la kukichoma moto lakini kwa bahati nzuri ni sehemu ndogo tu ya mlango huo ndiyo iliyoharibiwa. Duka moja la Waislamu lililo karibu na kituo hicho pia lilishambuliwa na watu hao na kupata hasara ndogo.
Masaa machache baada ya tukio hilo kituo cha Wahindu na kanisa la Wakristo pia vilishambuliwa kwa mada za moto na watu hao walio na chuki dhidi ya dini.
Licha ya matukio hayo ya kutia hofu lakini polisi ya New York imetangaza kuwa hadi sasa haijapata dalili yoyote inayounganisha matukio hayo wala wahusika wake. 928003