IQNA

OIC kuanzisha miradi ya kiuchumi mwaka 2012

15:43 - January 04, 2012
Habari ID: 2250968
Ekmeleddin Ihsanoglu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) amesema kuwa mwaka 2012 utashuhudia utangazaji wa miradi kadhaa ya kiuchumi katika nchi wanachama wa jumuiya hiyo.
Ameongeza kuwa mwaka huu pia OIC itashiriki katika Jukwaa la Masoko ya Hisa ya Ulimwengu wa Kiislamu.
Akizungumza na waandishi habari katika makao makuu ya OIC huko Jeddah, amesema kuwa kuna mpango pia wa kuanzisha Muungano wa Viwanda vya Kilimo vya Nchi za Kiislamu. Mpango mwingine ni wa kuhimiza biashara miongoni mwa vijana Waislamu, kustawisha maisha ya vijana vijijini na kutoa mafunzo kwa wakulima vijana.
Ihsanoglu ameongeza kuwa miezi ijayo itashuhudia kuanzishwa Kituoa cha Kibishara cha Kiislamu ambacho kitalenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi miongoni mwa nchi wanachama.
928156
captcha