IQNA

OIC yalaani mlipuko wa kigaidi wa Syria

11:05 - January 09, 2012
Habari ID: 2253780
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC jana Jumapili ilitoa taarifa ikilaani shambulio la kigaidi lililotokea mjini Damascus Syria hapo siku ya Ijumaa.
Katika taarifa hiyo, Ekmeleddin Ihsanoglu, Katibu Mkuu wa OIC amelaani vikali mlipuko huo wa kigaidi uliopelekea watu wengi kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa. Ametaka mazungumzo yafanyike mara moja kati ya serikali na wapinzani kwa ajili ya kutatua mgogoro uliopo. Amesema OIC daima imekuwa ikisisitiza kwamba mgogoro wa kisiasa wa Syria hauwezi kutatuliwa isipokuwa kupitia mazungumzo ya pande mbili na kwamba kutumiwa vitendo vya mabavu na ugaidi dhidi ya raia wasio na hatia hakusaidii lolote bali kunaharibu zaidi hali ya mambo.
Huku akiomboleza na familia za wahanga wa tukio hilo la kigaidi mwishoni mwa taarifa yake, Ihsanoglu amewataka wananchi na serikali ya Syria kushirikiana na kuimarisha umoja wao ili kukabiliana na changamoto tofauti zinazoikabili nchi hiyo. Mlipuko huo wa siku ya Ijumaa ulipelekea watu 26 kuuawa na wengine 60 kujeruhiwa. 931589
captcha