Afisa mwandamizi wa mpango huo Muhammad Bonyadi amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa usajili huo bado unaendelea.
Amesema kuwa miezi miwili baada ya kuanza usajili idadi kubwa ya waliojisajili ni kutoka mkoa wa Chaharmahal-Bakhtiari.
Kwa mujibu wa mpango huo wa Noor wanafunzi wanaoshiriki wanahifadhi nusu ya juzu ya Qur'ani Tukufu kwa kuhudhuria darsa za Qur'ani, CD n.k.
Bonyadi amesema mpango huo unalenga kuimarisha mafundisho ya Qur'ani, kustawisha kiwango cha kuhifadhi Qur'ani na kueneza utamaduni wa Qur'ani katika jamii.
Ameongeza kuwa kutakuwa pia na kitengo cha walimu na wafanyakazi wa Wizara ya Elimu katika mpango huo wa kuhifadhi Qur'ani.
931668