IQNA

Kanali ya Televisheni ya Kiislamu yaanzishwa Uswisi

15:02 - January 23, 2012
Habari ID: 2261403
Baraza Kuu la Waislamu Uswisi limetangaza mpango wa kuanzisha kanali ya televisheni ya interneti ya Kiislamu katikati ya mwaka huu wa 2012.
Kwa mujibu wa mwandisi wa IQNA barani Ulaya, Qaasim Illi Msemaji wa Baraza Kuu la Waislamu Uswisi amewaambia waandishi habari kuwa: 'Baada ya kuidhinishwa mradi wa msikiti mkubwa zaidi Uswisi katika mji wa Bern, baraza hili linalenga kuanzisha kanali ya kwanza ya televisheni ya Kiislamu katika interneti'.
Ameongeza kuwa, mbali na kurusha hewani hotuba za sala ya Ijumaa na mihadhara ya maulamaa wa Kiislamu, kanali hii itakuwa na mijadala ya kisiasa, kijamii na kiutamaduni. Aidha kutakuwa na kipindi maalumu chenye anwani ya 'Jarida la Wiki' ambalo litaangazia habari muhimu za Uswisi.
Qaasim Illi ameendelea kusema kuwa: 'Baraza Kuu la Waislamu Uswisi linapanga kutoa huduma kwa Waislamu nchini humo. Amesema kuna mpango wa kutoa 'Kadi ya Waislamu Uswisi' ambayo iwapo Muislamu ataiwasilisha katika taasisi kama vile za kitiba, kiutamaduni, michezo migahawa n.k atapata huduma kwa bei nafuu. 939498
captcha