IQNA

Misri, mwenyeji wa kongamano la kimataifa la Uchunguzi wa Vizuizi vya Mafunzo ya Qur’ani

18:44 - January 25, 2012
Habari ID: 2262376
Kongamano la kimataifa la Uchunguzi wa Vizuizi vya Mafunzo ya Qur’ani Tukufu limepangwa kufanyika tarehe 28 mwezi huu wa Januari nchini Misri chini ya usimamizi wa Baraza la Kiislamu la Kimataifa.
Kongamano hilo litafanyika kwa ushirikiano wa ofisi ya Jumuiya ya Kimataifa ya Hifdhi ya Qur’ani ya mjini Cairo na Jumuiya ya Kimataifa ya Vijana Waislamu chini ya kaulimbiu ya “Kuelekea kwenye Mustakbali Wenye Matumaini kwa Mahafidhi wa Qur’ani”.
Kongamano hilo litajadili maudhui mbalimbali kama vizuizi vya mafunzo ya Qur’ani na njia za kuviondoa, mchango wa mahafidhi wa Qur’ani Tukufu katika jamii na makundi yanayopangiwa mafunzo ya Qur’ani.
Maulamaa na wahubiri wanaojihusisha na masuala ya Qur’ani wa Misri na nchi nyingine duniani watashiriki katika kongamaano hilo.
Ripoti zinasema kuwa wanafunzi 80 kutoka nchi za Kiislamu wanoapata elimu katika Chuo Kikuu cha al Azhar ambao pia ni mahafidhi wa Qur’ani watashiriki katika kongamano hilo. 940541


captcha