Kongamano hilo la siku mbili linahudhuriwa na washiriki 1,500 kutoka nchi 73.
Katibu Mkuu wa kongamano hilo Dkt. Ali Akbar Velayati amewaambia waandishi habari kuwa washiriki watajadili nafasi ya vijana katika wimbi la Mwamko wa Kiislamu linaloshuhudiwa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskaini.
Kati ya malengo ya kongamano hilo ni kuhuisha malengo na thamani za Kiislamu kwa msingi wa Uislamu na Qur’ani, kurejesha heshima ya Kiislamu na kitaifa ya nchi za Kiislamu na kubuni ustaarabu mpya kwa msingi wa dini na mantiki. Aidha washiriki watabadilishana uzoefu wa harakati za kupigania uhuru na watajadili njia za kuarifisha demokrasia ya Kiislamu kama mbadala wa demokrasia ya kimagharibi.
Kongamano hili litakuwa ni la tatu la aina yake kufanyika mjini Tehran. Itakumbukwa kuwa mwezi Septemba mwaka jana wasomu na wanaharakati 700 kutoka nchi 80 duniani walishiriki katika Kongamano la Kwanza la Mwamko wa Kiislamu mjini Tehran. Aidha mwezi Novemba mwaka jana Tehran ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa Baraza Kuu wa Kongamano la Kimataifa la Mwamko wa Kiislamu. Kikao hicho kilihudhuriwa na wanazuoni kutoka nchi 17 za Kiislamu.
941793