IQNA

Maulidi ya Mtume (saw) kufanyika Ivory Coast

16:19 - January 29, 2012
Habari ID: 2264305
Maulidi ya Mtume Muhammad (saw) imepangwa kufanyika kwa shangwe katika mji mkuu wa Ivory Coast, Abidjan mnamo tarehe Nne Februari.
Kwa mujibu wa tovuti ya Fratmat maadhimisho hayo ya maulidi ambayo yamepangwa kuwashirikisha mamilioni ya Waislamu, yameyatarishwa na Baraza Kuu la Maimamu wa Jamaa la Ivory Coast. Usomaji Qur'ani, kasida na hotuba za kusifu na kubainisha maisha ya Mtume (saw) ni miongoni mwa ratiba za maadhimisho hayo ya kitaifa. Baraza lililotajwa limesema katika taarifa kwamba maadhimisho hayo yanafanyika kwa lengo la kuangazia maisha ya Mtume Mtukufu na kuonyesha jinsi Waislamu wanavyompenda Mtume huyo mtukufu. Limesema maadhimisho hayo ni fursa nyingine ya kuwakutanisha Waislamu na kuwadhihirishia walimwengu sura halisi ya Uislamu ambayo ni sura ya umoja, upendo, kuvumiliana na amani. 942608
captcha