Kongamano hilo liliandaliwa na Kamati Kuu ya Kimataifa ya Maandamano ya Ulimwengu kwa ajili ya Quds. Kongamano hilo ambalo lilifanyika chini ya usimamizi wa Salim al-Hos, Waziri Mkuu wa zamani wa Lebanon lilihudhuriwa na zaidi ya shakhsia wa kimataifa 35 kutoka mabara saba ya dunia. Wawakilishi wa kamati iliyotajwa kutoka mabara hayo na vilevile ulimwengu wa Kiarabu na Palestina pia walihudhuria kongamano hilo.
Akizungumza mbele ya washiriki, Salim al-Hos alisema kuwa kuandaliwa kwa makongamano kama hayo kuna umuhimu mkubwa katika kuimarisha mapambano dhidi ya mabeberu na walowezi wa Kizayuni huko Quds Tukufu na katika ardhi nyingine za Wapalestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.
Akizungumza katika hadhara hiyo, Ridha Fahmi, mkuu wa faili la Palestina katika harakati ya Ikhwanul Muslimeen ya Misri amesema kuwa Baraza Kuu la Kimataifa la Quds litaanzisha tawi lake hivi karibuni nchini Misri ambapo vijana wanamapinduzi na makundi ya kisiasa ya nchi hiyo yatakuwa na nafasi muhimu katika kuimarisha shughuli zake.
Katika taarifa yake ya mwisho, kongamano la Beirut lilisisitiza udharura wa kufanyika maandamano ya kimataifa ya kutetea Quds mnamo tarehe 31 Machi mwaka huu. 942756