Kwa mujibu wa tovuti ya Mosquee-lyon kongamano hilo la siku mbili litafanyika katika fremu ya shughuli za Taasisi ya Utamaduni wa Kiislamu inayofungamana na msikiti huo katika mwaka huu wa 2012 kwa lengo la kubainisha uhusiano uliopo kati ya Uislamu na sayansi au elimu za kisasa.
Taarifa iliyotolewa na waandaaji wa kongamano hilo inasema kwamba, mbali na kuwa Uislamu ni dini ya mbinguni, pia ni chanzo cha elimu mbalimbali na kiunganishi muhimu kati ya akili na hisia za mwanadamu jambo ambalo linaoonekana wazi katika maandishi na mijadala ya kielimu ya wasomi wa Kiislamu.
Inaendelea kusema kuwa utambuzi wa mwanadamu kuhusu nafsi yake na ulimwengu anamoishi ni utangulizi wa kumtambua Muumba wake ambaye ni Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala. Kwa kutilia maanani ukweli huo, wasomi na wataalamu watakaoshiriki katika kongamano hilo watajadili njia za kuunganisha elimu ya kisasa na mafundisho ya Kiislamu. 943326