IQNA

Maulidi ya Mtume (saw) kufanyika mjini Cairo

17:04 - February 01, 2012
Habari ID: 2266778
Maadhimisho ya Mtume Mtukufu (saw) yamepangwa kufanyika siku ya Ijumaa katika Msikiti wa ar-Rahman ar-Raheem mjini Cairo.
Kwa mujibu wa tovuti ya amlalommah, maadhimisho hayo ambayo hayakufanyika mwaka uliopita kutokana na matukio ya mapinduzi ya Misri, yamepangwa kufanyika mwaka huu na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya nchi hiyo.
Wanazuoni wa al-Azhar akiwemo Ahmad Khatib, Sheikh wa al-Azhar, Muhammad Abdul Fadhil al-Qausi, Waziri wa Wakfu wa Misri, Ali Jumua, Mufti pamoja na maafisa wengine wa serikali ya Cairo watahudhuria maadhimisho hayo.
Maadhimisho hayo yataanza kwa kisomo cha Qur'ani ambacho kitasomwa na Sheikh Farajallah as-Shadhili, Karii mashuhuri wa Qur'ani wa Misri na hutuba kutolewa na shakhisa mbalimbali akiwemo Ahmad Omar Hashim, mkuu wa zamani wa Chuo cha al-Azhar na Muhammad ad-Daftar mmoja wa wahadhiri wa chuo hicho.
Sambamba na kuadhimishwa maulidi hiyo ya Mtume (saw) Wizara ya Wakfu ya Misri itaandaa sherehe nyingine za maadhimisho hayo katika misikiti yote ya mikoa na wilaya mbalimbali za nchi hiyo.
Wakati huohuo Misri imepanga kushirikiana na nchi za Uturuki, Bahrain, Morocco na Syria katika kuandaa maadhimisho ya maulidi ya Mtume (saw) nchini Misri. 944609
captcha