IQNA

Wazayuni wataka Hosni Mubarak aokolewe!

20:15 - February 01, 2012
Habari ID: 2266850
Gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth limefichua kwamba kiongozi aliyeng'olewa madarakani wa Misri Hosni Mubarak amekuwa akiwaomba viongozi wa nchi mbalimbali duniani kufanya jitihada za kumnusuru na limewataka walimwengu wamsaidie dikteta huyo!
Shirika la habari la Nun limenukuu gazeti hilo likifichua jinsi Hosni Mubaraka anavyowalilia viongozi wa nchi mbalimbali ili wasimamishe kesi yake na uwezekano wa kuhukumiwa kifo yeye na watu wa familia yake.
Gazeti hilo limeeleza kusikitishwa na hali ya Mubarak, muitifaki mkubwa wa zamani wa Israel, na kuandika kuwa hukumu ya kifo itatolewa siku chache zijazo dhidi ya kiongozi huyo wa zamani wa Misri.
Limeandika kuwa hadi sasa Susan Mubarak, mke wa dikteta huyo wa zamani amewakabidhi mawakili wake barua 9 alizowaandikia viongozi wa nchi mbalimbali.
Yedioth Ahronoth limeandika kuwa katika barua hizo 9 alizowaandikia viongozi wa nchi za Kiarabu na Kimagharibi Mubarak amewaomba wafanye jitihada za kuwaachia huru watu wa familia yake na kuzuia hukumu ya kifo dhidi yake. 945359


captcha