IQNA

Umoja, haja mujimu ya umma wa Kiislamu

16:14 - February 05, 2012
Habari ID: 2268991
Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu ya Kiislamu Sheikh Mahmoud Ashur al Muslimi amesema kuwa umma wa Kiislamu unahitajia umoja na mshikamano zaidi katika kipindi hiki kuliko wakati wowote mwingine.
Al Muslimi amewataka viongozi kuwa macho mbele ya njama za maadui na kuimarisha umoja kati ya Waislamu.
Sheikh Ashur al Muslimi ametahadharisha pia kuhusu njama zinazofanywa na maadui kwa ajili ya kuzusha hitilafu na mifarakano katika umma wa Kiislamu.
Amesema kuwa maadui wa Uislamu daima wamekuwa wakifanya njama za kuzusha vita na uhasama kati ya Waislamu kwa kuzusha hitilafu na mifarakano baina yao. Amesisitiza kuwa dini tukufu ya Kiislamu inawaamuru wafuasi wake kulinda umoja na upendo baina yao.
Amewahimiza Waislamu kutosikiliza maneno ya makundi yanayowakufurisha baadhi yao akisema kuwa wafuasi wa makundi hayo hawaelewi vyema mafundisho ya Mtume Muhammad (saw).
Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu ya Kiislamu amesisitiza kuwa umma wa Kiislamu kama alivyosema Mtume (saw) ni kama mwili mmoja ambao maumivu ya kiungo chake kimoja husambaa na kuathiri viungo vyake vingine. 947693
captcha