IQNA

Sheikh Yazbak:

Njama za Marekani dhidi ya Syria zimegonga mwamba

16:25 - February 06, 2012
Habari ID: 2269824
Kushindwa kwa njama za kutaka kupasisha azimio dhidi ya Syria katika Baraza la Usalama ni pigo kubwa kwa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Hayo yamesisitizwa na Sheikh Muhammad Yazbak, Mkuu wa Kamati ya Masuala ya Kisheria ya Hizbullah katika sherehe za Maulidi ya Mtume (saw) mjini Baalabak kusini mwa Lebanon. Ameongeza kuwa wanamapambano wa Kiislamu hawatalegeza kamba katika hali yoyote ile.
Amesema yaliyofanyika katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ni kushindwa kwa wazi wazi mpango wa kuzusha fitina za kimadhehebu uliokuwa umetayarishwa na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Katika sherehe nyingine ya Maulidi ya Mtume (saw) iliyofanyika nchini Lebanon chini ya anwani ya "Muhammad (saw), Mtume wa Upendo na Amani kwa Ajili ya Mwanadamu", Ahmad Qatan ambaye ni kiongozi wa Jumuiya ya Kauluna Wal Amal amesema kuwa Marekani, utawala wa Kizayuni wa Israel na maadui wa Uislamu hawawatakii kheri watu wa Syria.
Ameongeza kuwa nchi kama Qatar na serikali nyingine za Kiarabu ambazo zinataka kuigawa Syria kupitia njia ya kuanzisha vita vya kimadhehebu na mauaji dhidi ya raia wa nchi hiyo zinataka kudhamini maslahi yao kwa kumwaga damu za watu wasiokuwa na hatia yoyote.
Viongozi hao wamesisitiza juu ya umoja na mashikamano wa Kiislamu. 948308
captcha