IQNA

Sherehe za Milad-un-Nabii SAW zafanyika Pakistan

12:16 - February 07, 2012
Habari ID: 2269990
Sherehe za Idd Milad-un-Nabii SAW zimefanyika kote Pakistan siku ya Jumapili tarehe 12 Mfunguo Sita Rabiul-Awwal na kuwakutanisha Waislamu wa matabaka mbalimbali ya jamii.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, gazeti la The Dawn limechapisha ripoti maalumu kuhusu sherehe hizo na kusema maulamaa na wanazuoni wamehutubia hafla za Maulid kote Pakistan. Miji mikubwa na midogo ya nchi hiyo imepambwa na mnasaba huo adhimu wa kukukumbuka siku ya kuzaliwa Mtume Muhammad SAW.
Sherehe za Maulid kitaifa zimefanyika katika mji mkuu wa Pakistan, Islamabad ambapo kulikuwa na dua maalumu kwa ajili ya ustawi, amani, umoja na udugu miongoni mwa wafuasi wa Mtume Muhammad SAW.
Siku ya Maulid ni siku ya mapumziko ya kitaifa Pakistan na usalama uliimarishwa kote nchini kwa mnasaba huu.
Rais wa Pakistan Asif Ali Zardari, Waziri Mkuu Yusuf Raza Gilani, Waziri wa Habari Firdous Ashiq Awan na viongozi wengine wametoa ujumbe maalumu kwa mnasaba wa Maulid.
Wameutaka wa Umma wa Kiislamu na mataifa ya Kiislamu kuimarisha umoja kwa mujibu wa mafunzo ya Mtume SAW ili waweze kukabiliana na changamoto zilizopo.
Hafla maalumu ya kusoma Qur'ani imefanyika katika Ikulu ya Rais wa Pakistan, 'Aiwan-e-Sadr' ambapo pia kulikuwa na dua maalumu kwa ajili ya umoja na kuunusuru Umma na taifa la Pakistan.
Halfa kuu ya siku ya Maulid ilikuwa 'Kongamano la Kitaifa la 'Seerat' ambapo Waziri Mkuu Yusuf Raza Gilani amehutubu na kusisitiza kuwa ni kwa kufuata mafundisho ya Mtume SAW ndio usalama na amani inaweza kupatikana duniani.
948483
captcha