IQNA

Waislamu Sudan kuadhimisha Maulidi ya Mtume SAW

21:29 - February 08, 2012
Habari ID: 2271526
Waislamu nchini Sudan wiki hii wanajiunga na wenzao kote duniani kuadhimisha sikukuu ya Maulidi ya Mtume SAW.
Barabara, misikiti na nyumba za watu binafsi zimepambwa kwa mataa yanayon'gara kwa mnasaba huu wa Maulidi.
Wasudani huadhimisha Maulidi kwa kusikiliza hotuba misikitini na maeneo ya kidini pamoja na mabarabarani. Katika hotuba zinazotolewa misikiti, makhatibu huelezea sira ya Mtume SAW. Aidha katika sherehe hizi hufanyika qiraa ya Qur'ani Tukufu na kuimbwa qasida za kuonyesha mapenzi kwa Allah na Mtume wake Mtukufu. Qurani na qasida husoma na makundi mbalimbali kuanzia usiku hadi asubuhi.
Kandoni mwa misikiti na barabra kuu, huwa na maduka maalumu ya kuuza tamutamu na viburudisho vya aina na rangi mbalimbali ambavyo hutengenezwa maalumu kwa mnasaba huu.
Aidha wageni Waislamu kutoka nchi mbalimbali duniani humiminika Sudan kusherehekea Miladun Nabi. Sherehe hizi hufanyika kwa njia maalumu nchini Sudan. Familia za Wasudani pia hujumuika majumbani kusherehekea Maulidi katika mazingira ya kirafiki ambapo wanaohudhuria husoma Qur'ani na kumsifu Mtume SAW.
949160
captcha