IQNA

Chama cha Kizayuni cha Likud chataka kuhujumiwa Masjidul Aqsa

14:45 - February 12, 2012
Habari ID: 2272535
Tovuti nyingi zinazofungamana na chama chenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia cha huko Israel cha Likud zimewataka waungaji mkono wa chama hicho kushambulia Masjidul Aqsa hii leo Jumapili tarehe 12 Februari.
Tovuti hizo zinasisitiza kwamba shambulio na hujuma hiyo inapasa kuandaa uwanja wa kujengwa kwenye mabaki ya msikiti huo, hekalu la Mayahudi.
Taasisi ya Wakfu na Turathi za Masjidul Aqsa imetangaza wasiwasi wake mkubwa kuhusiana na suala hilo na kuongeza kuwa tovuti zilizotajwa zinawachochea wanachama 1000 wa chama cha Likud kushambulia eneo hilo takatifu la Waislamu leo Jumapili ili kulitoa katika udhibiti wa Wapalestina.
Katika taarifa iliyosambazwa na taovuti hizo za Wazayuni, waungaji mkono wa chama cha Likud wametakiwa kutekeleza hujuma dhidi ya Masjidul Aqsa ili kuutoa katika udhibiti wa Wapalestina na kuandaa uwanja wa kujengwa hapo eti hekalu la Nabii Suleiman.
Katika kujibu uchochezi huo, Taasisi ya Wakfu na Turathi ya Masjidul Aqsa imewataka wakazi wa Quds Tukufu kuwepo daima katika msikiti huo mtukufu na kuzuia kuingia humo wavamizi wa Kizayuni.
Wametakiwa kutoruhusu utawala haramu wa Israel kutekeleza njama yake hatari na ya muda mrefu ya kutaka kuteka kibla hicho cha kwanza cha Waislamu. 951092
captcha