Kwa mujibu wa tovuti ya Islam Today, mbinu sita za kufundishia masomo hayo zitawasilishwa kwa wazazi ambapo watatakiwa kuchagua moja kati ya hizo kwa lengo la kutekelezwa mashuleni.
Kabla ya hapo waalimu watapewa mafunzo ya kutosha ili kuwawezesha kutoa mafunzo hayo kwa njia zinazofaa.
Masomo hayo yatahusiana na misingi ya dini za Kikristo, Kiorthodox, Kiislamu, Kiyahudi na Kibudha. Kufikia sasa majaribio ya mafunzo hayo yamefanyika katika maeneo 20 ya Russia na wanafunzi wapatao laki tatu tayari wamekwishashiriki katika mafunzo hayo ya majaribio.
Putin ametangaza habari hiyo katika hali ambayo anafanya juhudi za kugombea tena kiti cha rais wa nchi hiyo. 951752