Maadhimisho hayo ambayo yanaanza leo Jumatatu yataendelea hadi siku ya Jumatano. Maadhimisho hayo yameandaliwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini ya Algeria.
Katika kipindi hicho, ratiba mbalimbali zikiwemo za vikao na maonyesho ya Qur'ani zitatekelezwa ambapo wanazuoni na wahadhiri tofauti watazungumzia maudhui mbalimbali zinahusu kitabu hicho katakatifu cha mbinguni.
Baadhi ya maudhui hizo ni nafasi ya Qur'ani katika kuimarisha masuala ya kijamii na kifamilia ya mwanadamu wa leo.
Licha ya maudhui hizo mashindano ya hifdhi, tajwidi na tafsiri ya Qur'ani pia yatafanyika katika maadhimisho hayo.
Sherehe ya kuenzi na kuwashukuru washindi wa mashindano hayo itafanyika mwishoni mwa maadhimisho hayo. Mashairi na kasida za kumsifu Bwana Mtume (saw) pia zitaimbwa katika maadhimisho hayo ya kitaifa. 951730