IQNA

Hamas yataka Waislamu duniani wauhami Msikiti wa Al Aqsa

16:08 - February 13, 2012
Habari ID: 2273364
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu Palestina Hamas imetoa onyo kuwa Utawala wa Kizayuni wa Israel unataka kutekeleza njama zake za kuuhujumu Msikiti wa Al Aqsa na kuwalinda walowzi wa Kiyahudi.
Taarifa ya Hamas imeutaja Msikiti wa Al Aqsa kuwa ni 'mstari mwekundu' na kuonya kuwa hujuma yoyote dhidi ya msikiti huo itahesabiwa kuwa ni kutangaza vita dhidi ya Waarabu na Waislamu.
Hamas imetoa wito kwa Wapalestina wote kuungana katika kulinda Msikiti wa Al Aqsa.
Vikosi vya utawala ghasibu wa Israel vimekuwa vikizingira eneo la Quds ya Kale tokea Jumamosi Februari 11 kwa lengo la kuwawezesha walowezi wa Kizayuni wenye misimamo ya kufurutu mipaka kuvamia Msikiti Mtukufu wa Al Aqsa siku ya Jumapili. Njama hii ilizimwa na Wapalestina waliokuwa katika ua wa Msikiti huo.
Wakati huo huo tovuti ya habari ya Palestina ya Quds Net imemnukuu msemaji wa Hamas Ismail Ridhwan akisema, vitendo vyovyote vya hujuma za kuvunjia heshima msikiti wa Al Aqsa vitajibiwa vikali na harakati za mapambano za Palestina.
Amesema kuwa, taifa la Palestina na makundi mbalimbali ya muqawama kwa pamoja yanapaswa kusimama kidete dhidi ya hujuma yoyote itakayolenga Msikiti wa Al Aqsa.
Kiongozi huyo wa Hamas pia ametoa wito wa kufanyika mandamano katika nchi za Kiarabu na za Kiislamu ili kuonyesha hasira dhidi ya hujuma za utawala wa Kizayuni dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu.
952425
captcha