Gazeti la Arab News limeripoti kuwa, mashindano hayo yatafanyika kwa hima ya Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Saudia na chini ya usimamizi wa Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Sulaiman bin Abdul Aziz.
Mashindano hayo yataendelea kwa kipindi cha wiki moja.
Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Saudia Saleh Aal al Sheikh amesema kuwa mashindano hayo hufanyika kila mwaka kwa shabaha ya kueneza mafundisho ya Qur'ani na utekelezaji wake katika maisha ya mwanadamu. 952266