IQNA

Wasomaji bora wa Qur'ani kuchuana kesho Bandar Abbas, Iran

20:59 - February 13, 2012
Habari ID: 2273604
Mashindano ya 34 ya Qur'ani ya taifa nchini Iran yataanza kesho yakiwashirikisha makari bora 370 wa Qur'ani katika mji wa Bandar Abbas ulioko kusini mwa Iran.
Mashindano hayo yanayosimamiwa na Shirika la Wakfu na Masuala ya Kheri la Iran yataendelea hadi tarehe 19 Februari.
Makarii 370 waliofanikiwa katika awamu ya mchujo mikoani wakiwa ni wanaume 200 na wanawake 170, watachuana katika nyanja za kiraa, hifdhi, tartili ya Qur'ani na maana za aya za kitabu hicho kitukufu.
Tukio hilo kubwa zaidi la Qur'ani nchini Iran litaanza saa tatu asubuhi kwa wakati wa Iran na kusimamiwa na majaji wa kimataifa.
Katika kipindi chote cha mashindano hayo kutafanyika mahfali 100 za kiraa ya Qur'ani katika miji mbalimbali ya kusini mwa Iran ambazo zitawashirikisha wasomaji wa kimataifa wa Qur'ani Tukufu. 952401



captcha